HAWA NG`UMBI WEBSITE
  
Home
About Us
Contact Us
Subscribe
Invite A Friend
Publish Your Site
Article Search
 
Click here
if you find this
site offensive.
Digg Reddit Yahoo! Buzz Fark Facebook
     View Archives
Articles Per Page:

MKUU wa Wilaya ya Bukombe mkoani Shinyanga, Hawa Ng’umbi, ametangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Ubungo la jijini Dar es Salaam ambalo kwa sasa linashikiliwa na Charles Keenja aliyetangaza kutowania tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao. 

Kabla ya kuhamishiwa Bukombe, Ng'umbi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Makete, Iringa. 

Ng’umbi anakuwa Mkuu wa wilaya wa tatu kutoka mkoa wa Iringa kutaka kuachana na kazi ya kuwatumikia wananchi kupitia uteuzi unaofanywa na Rais na badala yake anataka kuwa mwakilishi wa wananchi bungeni. 

Wakuu wengine wa wilaya kutoka mkoani hapa, wanaoutaka ubunge ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Dk Athumani Mfutakamba aliyetangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Igalula mkoani Tabora ambalo kwa mwaka wa 20 sasa linashikiliwa na Tatu Ntimizi. 

Mwingine ni aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Njombe Charles Gishuri (anakwenda Kilindi) anayetaka kuwania ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini. 

Akitetea uamuzi wake wa kutaka kuwa mbunge na kuachana na ukuu wa wilaya endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo , Ng’umbi alisema anayo ndoto ya muda mrefu ya kutaka kuwa mwakilishi wa wananchi kupitia vikao vya bunge. 

Alisema ndoto yake hiyo ilianza mwaka 2000 alipoteuliwa kuwa Diwani wa viti Maalumu wa wilaya ya Kinondoni na haikushia hapo kwani mwaka 2005 aliomba nafasi ya Ubunge kupitia Viti Maalumu, lakini hakubahatika kupata nafasi hiyo baada ya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Janet Kahama na Janet Masaburi, walioteuliwa kuwa wabunge. 

Ng’umbi amesema,uzoefu wa miaka minne alioupata kwenye nafasi yake ya ukuu wa wilaya umemuongezea uwezo wa kisiasa na kwa kutambua kwamba anayafahamu fika matatizo mengi ya wakazi wa jimbo la Ubungo.


Current Articles

BARABARA ZAKARABATIWA KWA NGUVU ZA MAMA HAWA NG`UMBI
   Wilaya ya Makete inaweza ikaepukana na adha ya tatizo sugu la bara bara kufikia mwakani. Hayo yamefahamika mwishoni mwa wiki iliyopita wakati naibu waziri wa miundo mbinu Mh. Hezekia Chibulinje akipokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo akiwa ziarani wilayani Makete. Akisoma taarifa hiyo mkuu wa wilaya Bi. Hawa Ng’um...  More

MVOMERO Jimbo jipya lenye changamoto kibao
    Moja ya wilaya ambazo zimeanzishwa karibuni nchini ni Mvomero katika mkoa wa Morogoro, ikichukua pia jina la jimbo la uchaguzi. Ni wilaya ambayo ina sehemu tatu za hali ya hewa, kuanzia juu milimani, kati tambarare na mabondeni.  Pamoja na kuwa tajiri mkubwa wa ardhi, wilaya hii ina changamoto kubwa katika elimu na afya. Mkuu wa Wilaya ...  More

MTAZAMO WA WATU WA MAKETE KUHUSU UHAMISHO WA HAWA NG`UMBI
  

  Wananachi wa kata ya Matamba Wilayani Makete mkoani Iringa walimzuia aliyekuwa Mkuu wa Wilaya  kuondoka katika kijiji cha Matamba wakitaka kabla ya kuondoka kuwashughulikia viongozi wa kijiji wanaonyanyasa Wananchi. Wananchi hao walilazimika kumzuia mkuu huyo wa Wilaya ambaye amehamishiwa katika wilaya ya Bukombe mkoani Shinyanga kuo...

 More

Sponsor Links